Waziri akaribisha wawekezaji kutoka China

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji amewakaribisha wawekezaji kutoka China kuwekeza katika uzalishaji wa mafuta na bidhaa nyingine kwa matunda ya parachichi ili kuliongezea thamani zao hilo linalopatikana Tanzania.

Dk Ashantu amesema hayo leo, Julai 1, 2023 jijini Changsha alipokutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Shanghai Grenchain Bi Rossella Lyu na kusema pamoja na mambo mengine fursa hiyo itaongeza ajira kwa wananchi.

Kampuni hiyo ni miongoni mwa makampuni yanayonunua parachichi na pilipili kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya soko la China.

Kwa upande wake, Lyu ameeleza kwamba Kampuni yao ipo tayari kuanza kununua bidhaa za kilimo kutoka Tanzania sambamba na kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia bidhaa za vyakula (Cold Storage facilities).

Aidha, ameahidi kufanyia kazi wito wa Waziri Kijaji wa kuwekeza katika uongezaji thamani wa mazao ya kilimo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x