Waziri atumia bodaboda kukagua athari za mafuriko
MOROGORO; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki kukagua miundombinu ya barabara zilizoathiriwa na mafuriko Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro.
Athari za mafuriko katika Mji wa Malinyi zimechangiwa na maji ya Mto Furua kusambaa na kuharibu kwa kiwango kikubwa Barabara ya Igawa-Malinyi, Lugala- Misegese ,Njiapanda -Malinyi na kufanya magari kushindwa kupita, hivyo kuathiri shughuli mbalimbli za kijamii na kiuchumi.