Waziri auawa kwa risasi na mlinzi wake

WAZIRI wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake asubuhi hii akiwa nyumbani kwake Kyanja Kampala.

Naibu msemaji wa polisi wa Kampala, Luke Owoyesigire amethibitisha.

“Ndiyo. Tukio limetokea Kyanja. Mwanajeshi amempiga risasi bosi wake,” Owoyesigire aliambia chapisho la ‘Daily Monitor.’

Spika wa Bunge, Anita Among, pia alithibitisha kifo cha waziri huyo alipokuwa akiongoza kikao cha mashauriano leo asubuhi.

“Leo asubuhi nimepata taarifa za kusikitisha kuwa Mh Engola amepigwa risasi na mlinzi wake na baadae kujipiga risasi. Roho yake ipumzike kwa amani,” Among alisema.

Waziri wa Jinsia, Betty Amongi ni miongoni mwa maafisa wa serikali ambao tayari wamefika nyumbani kwa Engola huko Kyanja.

Habari Zifananazo

Back to top button