Waziri Aweso ahimiza ajenda ya maji Afrika

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amehimiza umuhimu wa Afrika kuipa hadhi ajenda ya maji kwa kuimarisha uwekezaji katika sekta hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo katika katika Mkutano wa 13 wa Kamati ya Utendaji ya Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW), jijini Windhoek, Namibia.

Amesema maji ni kiungo cha maendeleo kupitia usalama wa chakula, usalama wa nishati, afya ya jamii, mazingira, uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, misitu na viwanda.

Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali kuhusu dira ya maji ya Afrika ya mwaka 2025, ajenda ya maji Afrika, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwekezaji katika sekta ya maji.

Waziri Aweso amesisitiza kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana na AMCOW, katika kuboresha usimamizi wa rasilimali za maji, usambazaji maji na usafi wa mazingira nchini.

 

Habari Zifananazo

Back to top button