WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameshiriki katika mjadala wa Uongozi na Usimamizi wa Masuala ya Maji katika mkutnao ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaoendelea New York Marekani.
Mjadala huo ambao uliandaliwa na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na Afrika Kusini pamoja na mashirika mbalimbali ikiwemo GWP, UNICEF na UNDP, ulihudhuriwa na mgeni Rasmi ambaye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa GWPSA na Mwenyekiti mwenza wa Jopo la Viongozi maarufu kuhusu uwekezaji katika sekta ya maji.
Katika mchango wake, Aweso alibainisha uongozi imara wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika agenda ya kwa kuongeza msukomo na utashi wa kisiasa, kuongeza bajeti ya maji; na kuimarisha taasisi zinazohusiana na usimamizi wa huduma za maji na utekelezaji wa Miradi ya Maji.
Katika kutekeleza hilo, Tanzania inatekeleza Programme ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 6.47 na mwezi Mei 2023 itazindua Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji (Tanzania Water Investment Programme 2023-2030).
Kupitia mjadala huo, Tanzania imeongeza wadau mbalimbali wa kushirikiana nao katika Sekta ya Maji.
Comments are closed.