Waziri Kairuki aeleza vipaumbele 5 vya TAMISEMI bungeni

TANGU ateuliwe kuwa mbunge na hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angelah Kairuki hajapata fursa ya kuzungumza jambo lolote juu ya eneo lake la kazi.

Kutokana na hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amelazimika kumsimamisha leo asubuhi Bungeni ili aseme jambo kuhusu ofisi yake mpya ya TAMISEMI.

Baada ya kupata fursa hiyo, Waziri Kairuki ameeleza mambo matano ambayo atayashughulikia kuhakikisha kuwa TAMISEMI inawahudumia wananchi kwa uhakika.

buy wellbutrin online thececonsultants.com/files/thumbnails/png/wellbutrin.html no prescription pharmacy

Amewaahidi wabunge kuwa wizara yake itaweka nguvu katika kuimarisha mifumo ya kitaasisi kwa kuwa viongozi wanaoteuliwa, akiwemo yeye mwenyewe, wanabadilika hivyo ni wakati sasa wa kuimarisha mifumo ya kitaasisi ili yeyote atakayepata nafasi ya kuongoza kuleta ufanisi.

buy neurontin online drweitz.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/neurontin.html no prescription pharmacy

Kwa mujibu wa Waziri, eneo jingine la kipaumbele ni  kuimarisha mifumo ya kihasibu katika halmashauri zote nchini pamoja na kuzuia upotevu wa fedha za umma.

buy buspar online thececonsultants.com/files/thumbnails/png/buspar.html no prescription pharmacy

Kuhusu makusanyo, Waziri Kairuki amesema TAMISEMI itaweka nguvu katika makusanyo ya halmashauri ikiwemo kupitia makadirio ya mapato dhidi ya vyanzo vilivyopo kwani baadhi zimekuwa zikijiwekea malengo chini ya kiwango na hatimaye kuonekana wamefanya vema.

Habari Zifananazo

Back to top button