Waziri Kairuki akabidhiwa ofisi Tamisemi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki, amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Innocent Bashungwa ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Hafla hiyo ya makabudhiano imefanyika Makao Makuu wa Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 6, Oktoba 2022.

Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia, Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Kairuki kuwa Mbunge na Waziri wa Tamisemi, huku Bashungwa akiteuliwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button