Waziri Kairuki atembelea ofisi za DART

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki, ametembelea Ofisi za Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dar es salaam na kupokelewa.

Katika ziara hiyo amepokelewa na Mkurugenzi wa DART, Dk Edwin Mhede, ambapo atazungumza na Menejimenti ya wakala pamoja na watumishi wa DART.

Kesho Waziri Kairuki anatarajiwa kutembelea miradi ya DAR kwa kukagua vituo vya mabasi na huduma zinazotolewa kuanzia kituo cha Mabasi cha Kimara mpaka Mbagala.

Habari Zifananazo

Back to top button