WAZIRI ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula, amekasirishwa na utendaji kazi mbovu na kutokuwa na ushirikiano baina makamishina wa ardhi na viongozi wengine.
Dk Mabula pia amemuelekeza Katibu wa Wizara hiyo, kuhakikisha anaanza kuchukua hatua mara moja kwa makamishna wasaidizi wa ardhi, wale walioshindwa kukidhi matarajio pamoja na wasaidizi wao.
Akizungumza leo jijini Da es Salaam katika kikao cha makamishina wasaidizi wa ardhi kutoka mikoa mbalimbali, ameeleza kuwa makamishana hao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea, wanaogopana, wanalindana na hivyo kuathiri utendaji wa kazi.
“Mikoa ambayo tunakamilisha taratibu za kinidhamu kwa watumishi siku za hivi karibuni ni Mbeya, Dar es Saaam, Mwanza, Arusha na Lindi,” amesema.
Amesema pamoja na hatua za kinidhamu, ambazo zimechukuliwa kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kuwaachisha kazi Mbeya watatu na Dodoma wanne, ameagiza hatua zichukuliwe kwa mikoa mingine.
“Kwa mashauri ya kinidhamu ambayo yanaendelea naelekeza yakamilishwe haraka, mikoa ambayo tunakamilisha taratibu za kinidhamu kwa watumishi siku za hivi karibuni ni Mbeya, Dar es Saaam, Mwanza, Arusha na Lindi,”amesema Dk Mabula.
Pia amesema wamebaini kuwa wapo watumishi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye uthamini wa mali, ambapo majina yao wameyapata na watachuku hatua za haraka.
“Siridhishwi kabisa na utendaji wa Mkurugenzi wa TEHAMA, naelewa Katibu Mkuu analifanyia kazi, naelekeza lifanyiwe kazi kwa haraka na muda mfupi,”amesisitiza.
Amewataka wakurugenzi kuacha kukaa ofisisi na kusubiri taarifa, badala yake wafikie na kuangalia na kujiridhisha na kutoa ushauri.