Waziri Mbarawa amshukuru Samia miradi uchukuzi

DAR ES SALAAM; Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimbali ya uchukuzi na ameahidi kusimamia miradi hiyo kwa uadilifu kwa maslahi mapana ya nchi.

Waziri Mbarawa amesema hayo leo Machi 26, 2024 katika mapokezi ya ndege mpya ya abiria aina Boieng 737-9MAX katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema wizara itaendelea kusimamia na kutekeleza usimamiaji wa sera za wizara ya uchukuzi na wizara itaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa taasisi zilizokuwa chini yake, ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Advertisement

Amesema serikali imenunua ndege mbili kwa ajili ya mafunzo ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa marubani ambao watakwenda kwenye soko la ajira, ili kupunguza uhaba wa ajira nchini.
Pia amesema chuo hicho kimewezeshwa mitambo na vifaa ya kisasa kwa ajili ya kutoa shahada na stashahada ya uhandisi wa ndege, ili kuzalisha wahandisi bora watakaoingia kwenye soko la ajira.