Waziri Mkuu afurahishwa huduma Muhimbili

WAZIRI Mkuu, Kassim Mjaliwa amefurahishwa na utoaji wa huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Majaliwa ameyasema hayo leo Julai 24, 2023 alipotembelea hospitali hiyo na kupata fursa ya kuwasalimia wagonjwa.

“Nimefurahishwa sana jinsi mlivyoboresha huduma, wakati napita kusalimia baadhi ya wagonjwa wamenieleza kuridhishwa na huduma wanazopatiwa, hii inatia moyo sana.”amesema Majaliwa.

Sambamba na hilo, Majaliwa amefurahisha pia na uboreshwaji, mwonekano wa mazingira na majengo ya hospitali hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa menejimenti itaendelea kuimarisha huduma zake katika nyanja mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button