Waziri Mkuu afutwa kazi baada ya wiki moja

RAIS wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo amemfuta kazi Waziri Mkuu, Geraldo Martins wiki moja baada ya kumteua katika nafasi hiyo hata hivyo sababu za kutenguliwa hazikuwekwa wazi.

Martins aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu Desemba 12 huu. Katika taarifa ya uteuzi iliyosomwa na mshauri wa Rais Sissoco, Fernando Delfim da Silva alimteua Rui Duarte de Barros kama Waziri Mkuu mpya.

Rui Duarte de Barros ni mwanachama wa Bunge kutoka Chama cha Afrika kwa Uhuru wa Guinea na Cape Verde (PAIGC), ambayo sasa inaongoza umoja wa upinzaji.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa akihudumu kama Rais wa Baraza la Utawala la Bunge la Kitaifa.
Rui de Barros aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Guine wakati wa serikali ya mpito kati ya Mei 2012 na Juni 201

Habari Zifananazo

Back to top button