Waziri Mkuu akagua miradi Itilima

Waziri Mkuu akagua miradi Itilima

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Njalu katika Kijiji cha Kimali, Kata ya Nyamalapa, wilayani Itilima, mkoani Simiyu na kuagiza shule hiyo iwe ya mfano.

Pia Waziri Mkuu alizindua mradi wa ghala la kuhifadhi mazao ya chakula katika Kijiji cha Ikindilo, wilayani Itilima ambao uliogharimu Sh milioni 990, ujenzi wa ghala hilo umelenga kudhibiti sumukuvu kwenye mazao ya chakula kwa kuongeza ufanisi katika uhifadhi wa mazao.

Advertisement

Waziri Mkuu amefanya mikutano miwili mikubwa ya hadhara na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Kimali na Ikindilo vilivyoko wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *