Waziri Mkuu ampongeza Dk Tulia urais IPU
WAZIIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameungana na Rais Samia kumpongeza Spika wa Bunge, Dk Tulua Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya Dunia-IPU.
PM Majaliwa ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.
“Ushindi huu ni kielelezo cha imani kubwa ambayo Mataifa mengi Duniani wanayo juu ya nchi yetu na wewe mwenyewe,”
“Ninakutakia kheri katika jukumu hili linalounganisha Mataifa yetu pamoja ili kujadili mwelekeo chanya wa Dunia.” ameandika Waziri Mkuu Majaliwa.