Waziri Mkuu amtaja Aziz Ki akizipongeza Simba, Yanga

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa hoja ya kuahirisha Bunge leo jijini Dodoma huku akizipongeza timu za Simba na Yanga kwa kuingia hatua za makundi katika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.

Mbali na Simba kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikitinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho, Waziri Mkuu amezipongeza Serengeti Girls, Tembo Warriors na Simba Queens kwa kufika hatua za juu katika mashindao timu hizo zilizoshiriki hivi karibuni.

“Kipekee nimpongeze [Stephanie] Aziz Ki aliyefunga bao pekee huku akisema Yanga imeweka historia kwa kuiondoa moja ya timu zilizopo Kaskazini mwa Bara la Afrika.

Wakati akizungumza hilo, Wabunge wanaoshabikia klabu hizo kongwe walikuwa wakipiga meza wakati timu hizo zikitajwa na Waziri Mkuu.

Habari Zifananazo

Back to top button