IDADI ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa VVU/UKIMWI imepungua kutoka wastani wa maambukizi mapya 100,010 mwaka 2010 hadi kufikia 54,000 mwaka 2021.
Akizungumza leo mkoani Mtwara Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa na jitihada juu ya mapambano dhidi ya uongojwa huo ambapo mwaka 2001 Serikalii ilielekeza suala la Ukimwi kuwa ni ajenda ya Kitaifa na ujumbe wa kudumu katika mbio za Mwenge wa Uhuru mpaka hapo ungonjwa huo utakapotokomezwa.
Hata hivyo ,Vifo vinavyotokana na Ukimwi vimeshuka mpaka 65,000 kwa mwaka 2010 hadi 29,000 mwaka 2021. Amesema kushuka kwa vifo hivyo kunatokana na kuimarika na kusambaa kwa huduma za matibabu ya ARV Nchini lakini pia elimu ya kujikinga na maambukizi hayo kwa Watanzania.
’Maamuzi haya yalitokana na ukweli kwamba katika miaka 1990 na mwaka 2000 maambukizi mpya VVU kwa mwaka yalikuwa ni ya kutisha na yalikadiliwa kufikia takribani Watu laki 2 na kusababisha vifo vingi kwa Watanzania’’,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania hao kuhakikisha wanaepukana na maambukizi ya Ukimwi na kuchukua taadhari zote na kwa kupitia mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 wananchi watakumbushwa suala zima la kuchukuwa tahadhari dhidi ya maambukizi hayo ya Ukimwi.
‘’Hii ni ajenda ya kudumu kila mbio za mwenge tutahakikisha tunapambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, ubaguzi, unyanyapaa dhidi ya Waviuu kama hatua muhimu ya kupammbana na janga hili la Ukimwi Kitaifa’’,