Waziri Mkuu atembelea bandari ya Mtwara

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea Bandari ya Mtwara ambapo pia amekagua gati mpya yenye urefu wa mita 300 ikiwa na uwezo wa kuhudumia meli yenye uzito wa hadi tano 65,000.

Ujenzi wa gati hiyo umeiwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena katika bandari ya Mtwara kutoka tani laki nne hadi kufikia zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka.

Ujenzi gati hiyo umegharimu shilingi bilioni 157.8

Habari Zifananazo

Back to top button