Waziri Mkuu atoa maagizo Wizara ya Madini

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshilikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa.

Majaliwa amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi.

Ametoa agizo hilo leo Oktoba 07, 2025 alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi.

SOMA: Majaliwa ataka sekta ya madini kuwa na tija kiuchumi

“Kampuni ya Paco Gems tangu 2009 mpaka leo hakuna maendeleo, tunatoka Utanex pale Chunyu, wameshalipa fidia tangu 2012 lakini mpaka leo hii hakuna maendeleo yoyote, ipo kampuni ya Nachu ambayo ilipata heshima ya kusaini mkataba mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo hii wamepotea na hakuna taarifa.”

Majaliwa ameipongeza kampuni ya Huaer International Limited ambayo imefanikiwa kuanza mchakato wa uwekezaji ndani ya kipindi kifupi baada ya kupata vibali vyote muhimu.

“Kampuni yako ambayo imeanza ukaguzi mwaka 2024, ukapata matokeo mwaka huohuo na kuomba vibali mwaka huohuo, leo mmeanza utekelezaji wa ujenzi na mmefikia hatua hii, ninyi mnapaswa kupongezwa na mnapaswa kuwa mfano wa makampuni haya mengine tata.”

Kadhalika, Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa kampuni hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuzalisha ajira kwa Watanzania kupitia uwekezaji.

“Kampuni hii ndiyo inaanza na inaendelea na ujenzi mtakapokamilisha mtatoa nafasi ya Watanzania na Wana Ruangwa kupata ajira hapa.”

Pia, Majaliwa ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania waliopata nafasi ya kufanya kazi katika kampuni hiyo kufanya kazi kwa bidii, weledi, nidhamu na uaminifu “Tunahitaji kuwahakikishia hawa wawekezaji kwamba tunaajirika na tunaweza kufanya kazi hizi.”

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. I honestly didn’t expect much when I first tried this, but here I am making around 6,854/USD a month just by working online a few hours a day from home. It’s not a get-rich scheme, just something steady that’s been working for me quietly in the background. If you’ve been looking for something consistent like I was, here’s what I started with:
    👉 https://www.jobs67.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button