Waziri Mkuu atoa maelekezo hewa ya ukaa

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi kupitia upya mikataba ya biashara ya hewa ukaa inayofanyika katika Halmashauri hiyo, ili serikali na wananchi waweze kunufaika kupitia biashara hiyo.

Akizungumza wilayani Tanganyika katika ziara ya siku tatu anayoifanya Mkoa wa Katavi, aliyoianza leo Desemba 12, 2022 Waziri Mkuu Majaliwa amitaka halmashauro hiyo kurejea upya mikataba hiyo na Kampuni ya Carbon Tanzania Limited kwa kushirikiana na taasisi ya Tuungane wanaotekeleza mradi huo.

Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi hundi ya Sh billioni 8 kwa vijiji vinavyonufaika na mradi huo wa hewa ukaa katika Kijiji cha Kagunga, wilayani Tanganyika.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata, bado kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa wananchi kuhusu biashara hiyo.

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa hewa, ukaa Marc Baker ameeleza maeneo ambayo wanatekeleza mradi huo ni Vijiji vya Lugonesi, Mwese, Lwega, Bujombe, Kapanga, Katuma, Mpembe na Kagunga.

Waziri Mkuu pia amekagua ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Katavi na kuacha maagizo kwa viongozi wa mkoa kuhakikisha ifikapo Januari 1, 2023 hospitali inaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Habari Zifananazo

Back to top button