Waziri Mkuu DR Congo ajiuzulu

WAZIRI Mkuu wa DR Congo, Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu.

Lukonde aliwasilisha ombi la kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi. Sasa atajiunga na bunge kama mjumbe wa bunge hilo.

“Kujiuzulu kumekubaliwa. Hata hivyo, rais ameiomba serikali (ya Lukonde) kuendelea kushughulikia masuala yaliyopo” hadi serikali mpya itakapoundwa, ofisi ya rais ilisema katika taarifa nyingine.

Advertisement

Taarifa hiyo haikuweka wazi sababu za kujiuzulu kwake.

Lukonde aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa madini mnamo Februari 2021.