WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Kitaifa zitakazofanyika Aprili Mosi mkoani Mtwara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako ametoa taarifa hiyo leo 30 Machi 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mwenge huo.
Amesema baada ya uzinduzi mwenge huo utakimbizwa katika mikoa 31 , halmashauri 195 za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kwa siku 195.
Amesema kwake kipindi chote cha kuukimbiza Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha umoja, amani na mshikamano wa kitaifa pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.
“Katika mikoa na Halmshauri za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakapokuwa ukikimbizwa ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge kwa mwaka utakuwa ni TUNZA Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji Kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa,” amesema.
Waziri amesema ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu unazingatia umuhimu wa kuhifadhia Mazungumzo na Utunzaji wa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa Viumbe His na Uchumi wa Taifa.