Waziri Mkuu mstaafu Pakistan akamatwa

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan amekamatwa nje ya Mahakama ya Islamabad leo Mei 9, 2023.

Taarifa ya iliyotolewa leo na mtandao wa ‘THE TIMES OF INDIA’ imeeleza kuwa mwenyekiti huyo wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf alikuwa ameenda kutafuta dhamana dhidi ya kesi zilizosajiliwa dhidi yake.

Khan alipangwa kufika mbele ya Mahakama Kuu ya Islamabad katika kesi ya uasi, rushwa na nyingine inayohusu mashtaka ya kujaribu kuua.

Habari Zifananazo

Back to top button