WAZIRI Mkuu wa Uingereza Liz Truss alilazimika Jumatatu kubadilisha mipango ya kupunguza kiwango cha juu zaidi cha ushuru wa mapato ambayo yaliibua uhasama katika chama chake na kuchochea msukosuko katika soko la fedha.
Truss, na waziri wake wa fedha Kwasi Kwarteng, walitangaza “mpango mpya wa ukuzaji uchumi” mnamo Septemba 23 ambao ungepunguza ushuru na udhibiti, kwa kuongeza ukopaji mkubwa wa serikali ili kuondoa mdororo wa uchumi uliokwama kwa miaka mingi.
Lakini mpango huo uliibua mzozo wa imani ya wawekezaji kwa serikali, na kuongeza thamani ya pauni na bei ya dhamana za serikali na hivyo kuyumbisha soko la kimataifa kiasi kwamba Benki ya Uingereza ililazimika kuingilia kati na mpango wa pauni bilioni 65 (Sh trilioni 169.7) kuinua masoko.
Wakati kuondolewa kwa kiwango cha juu cha ushuru kilikuwa karibu bilioni 2 kati ya mpango wa kupunguza ushuru wa pauni bilioni 45, (kipengele cha kuvutia zaidi cha kifurushi cha fedha ambacho kilipaswa kufadhiliwa na mikopo ya serikali), Waziri wa Fedha Kwarteng hakueleza jinsi mpango huo utakavyolipwa kwa muda mrefu.
Saa chache tu baada ya Truss kwenda kwenye runinga ya BBC kutetea sera hiyo, Kwarteng alitoa taarifa akisema anakubali imekuwa kikwazo kutoka kwa juhudi pana za kusaidia kaya wakati wa baridi kali.
“Kutokana na hilo, natangaza kwamba hatuendelei na kufuta kiwango cha kodi cha asilimia 45. Tumewaapata, na tumewasikiliza,” alisema katika taarifa hiyo.