Waziri Mkuu wa zamani ruksa kurejea Ivory Coast

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Ivory Coast, Guillaume Soro aliyekuwa uhamishoni sasa anaweza kurejea nchini humo.

Msemaji wa serikali ya Ivory Coast , amesema ni mfumo wa haki ndio utakaoamua juu ya utekelezaji wa hukumu za Soro nchini humo.

“Anaweza kurejea nchi iko wazi.

Wote waliotaka kurudi wamerejea, na tunawaona wakishiriki mikutano ya kisiasa,” amesema.

Kiongozi wa zamani wa waasi na Waziri Mkuu alitangaza karibu wiki mbili zilizopita kwamba anamaliza uhamisho wake na kurejea Afrika.

Guillaume Soro aliondoka Ivory Coast mwaka wa 2019 baada ya kutofautiana na Rais wa sasa Alassane Ouattara.

Mnamo 2020, alihukumiwa bila kuwepo kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za umma na mwaka mmoja baadaye, kifungo cha maisha kwa kuhatarisha usalama wa Serikali.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button