Waziri Ummy aunga mkono mtumishi wa afya kusimamishwa

KITENDO cha Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kumsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kuvule kimeungwa mkono na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu. Mtumishi huyo amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia miongozo ya udhibiti wa magonjwa.

Kupitia video fupi iliyosamba kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni, alionekana mtumishi wa kituo hicho akiosha vifaa tiba vya hospitalini katika hali isiyofaa hivyo kutafsiria kukiuka mingozo ya afya.

Licha ya pongezi za Waziri Ummy kwa mkurugenzi huyo, pia alikemea kitendo hicho na kwamba hakikubaliki na kusisitiza ni ukiukwaji wa maadili ya taaluma hivyo kuna uzembe kwenye suala ya usimamizi wa miongozo ya afya katika kituo hicho

“Tumeona juzi kule Dar es salaam, mtumishi anaosha vyombo vya hospitali kwa maji ya baridi na kuanika juani, sijawahi kuona na nimefurahi kuona kuna hatua imechukuliwa na mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumsimamisha kazi mganga mfawidhi kwa kushindwa kusimamia majukumu yake” alisema Waziri.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button