Waziri wa ulinzi China aondolewa

WAZIRI wa Ulinzi wa China, Li Shangfu amefutwa kazi leo ikiwa ni miezi miwili baada ya kutoonekana hadharani bila maelezo yoyote rasmi.

Shangfu pia ameondolewa kwenye nyadhifa zake kama mjumbe wa Tume Kuu ya Kijeshi chombo chenye nguvu kinachoongozwa na Rais wa China Xi Jinping.

Uamuzi huo uliidhinishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la nchi hiyo, Bunge la Wananchi, kulingana na taarifa ya Shirika la Habari la CNN nchini China.

Li, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mwezi Machi, hajaonekana hadharani tangu mwishoni mwa mwezi Agosti, na hivyo kuchochea uvumi mkubwa kuhusu hatma yake.

Kutoweka kwa jenerali huyo kunafuatia mfululizo wa misukosuko isiyoelezeka ya wafanyikazi ambayo imekumba safu ya juu ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Qin Gang mnamo Julai.

Habari Zifananazo

Back to top button