WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov amekimbizwa katika Hospitali ya Bali nchini Indonesia baada ya jana kuwasili nchini humo kushiriki mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiuchumi Duniani, G20.
Lavron amefika katika mkutano huo kumuwakilisha Rais, Vladimir Putin.
Taarifa ya Shirika la Habari la ‘Associated Press’ limedai kiongozi huyo anasumbuliwa na tatizo la moyo, ingawa taarifa za Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imeziita taarifa hizo kama uzushi.