MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba, amewataka wafanyabiasha wanaojihusisha na biashara haramu za magendo na dawa za kulevya ‘Wazungu wa Unga’, kujisalimisha, kwani hakuna mhalifu yeyote mkoani humo atabaki salama.
Amesema siku zote watu walizoea kuwa serikali inashughulika na watumiaji, ila kwa sasa watashughulika na wauzaji na wasafirishaji, ili kutokomeza vitendo vya uhalifu.
Ameyasema hayo, wakati akishuhudia ushushwaji wa mzigo haramu wa magendo wa roba za vitenge zaidi ya 180 zilizokuwa zikisafirishwa kwenye malori mawili yenye namba za usaili T382 DLM na T364 DDM yaliyokuwa yakisafirisha mawe aina ya Tangastone kuelekea Dar es Salaam kutokea mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga.