DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema hatoacha kumtaja na kumsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyohakikisha miradi ya maendeleo nchini inasonga mbele.
Akiwa katika sherehe za kupokea ndege mpya aina ya Boeing 737-Max 9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Chalamila amehoji kwa nini alaumiwe kwa kumtaja Rais Samia mara kwa mara.
“Mnataka niseme asante ndugu Mbowe kwa maendeleo?
” Amehoji Chalamila.