Weghorst, Sabitzer kurejea walipotoka

HUENDA kocha wa Manchester United, Eric Ten Hag hajaridhishwa na viwango vya wachezaji Wout Weghorst kutoka Burnley na Marcel Sabitzer kutoka Bayern ambao wote walikuwa kwa mkopo United.

Kutoridhishwa huko kunatokana na uamuzi wa klabu hiyo kuamua kuachana na wawili hao kurejea walipotoka. Mtandao wa Mail kutoka Uingereza umeripoti.

Weghorst na Sabitzer walijiunga na United kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari, hata hivyo wameiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Carabao Cup, kufika fainali ya Kombe la FA na kufuzu Ligi ya Mabingwa

Habari Zifananazo

Back to top button