Wekeni wenye sifa sekta ya ununuzi

WAAJIRI wote nchini  wametakiwa kuhakikisha wanaweka watu wenye sifa kusimamia sekta ya ununuzi na ugavi, ili kuondoa lawama katika miradi inayotekelezwa chini ya viwango.

Akifungua kongamano la 13 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi jijini Arusha, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, amesema baadhi ya taasisi za serikali na sekta binafsi zinaajiri au kupachika watu wa ununuzi wasio na sifa.

Amesema athari ya jambo hilo ni kuleta hasara katika miradi mbalimbali, kisha lawama zinamwagukia ofisa ununuzi, ambaye hakuhusika kusimamia au si mtu sahihi kusimamia miradi.

Amesisitiza bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), kusimamia vyema nidhamu katika fani huyo, ili iendelee kuheshimika zaidi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button