“Wekezeni kwenye maadili ya watoto”
JUMUIYA ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salam, imetahadharisha jamii kuwekeza zaidi katika malezi bora ya watoto hatua ambayo itasaidia kuondoa tatizo la mmomonyoko wa maadili jambo ambalo limeendelea kushika kasi nchini.
Onyo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, mkoa wa Dar Es Salam Khadija Ally Saidi wakati wa ziara ya kukagua uhai wa jumuiya hiyo na chama katika kata sita za jimbo la Kibamba, wilaya ya Ubungo.
Alisema jamii inawajibu mkubwa wa kuwekeza katika malezi bora ya watoto ambayo Kwa kiasi kikubwa yameathiriwa na utandawazi na kwamba iwapo hatua za makusudi hazitachukiliwa kudhibiti hali hiyo taifa litazalisha vijana wasio kuwa na maadili.
“Kwa Sasa tunaona Kuna wimbi kubwa la watoto wetu kukosa maadili kutokana na matumizi ya sio sahihi ya mitandao ha kijamii…sisi kama wazazi na jamii tunawajibu mkubwa ambao tunapaswa kutekeleza katika malezi bora ..tuwafundishe watoto wetu kujiamini na kujitambua pia tusipofanya hivyo tunazalisha bomu katika taifa letu”alisema
Aidha alisema vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikitokea kutokana na mmonyoko mkubwa wa maadili jambo ambalo limechingiwa na jamii kutokuwa na hofu ya Mungu na kukosa utu na kwamba jumuiya hiyo bado itaendelea kusimamia masuala yote ya sera malezi.
Mbali na hilo alitoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho hususani wa jumuiya hiyo kufuata kanuni na misingi yote ya chama hicho ikiwemo kukaa vikao vya mara Kwa mara jambo ambalo litasaidia Chama hicho kuendelea kuwa hai na kuwa na wananchama wengi zaidi.
Katika hatua nyingine mwenye kiti huyo lizindua orogramu ya usajili wa wananchama Kwa njia ya kielekronini na kupokea zaidi ya wananchama wapya 20 kutoka katika vyama vingine vya siasa.
Naye Diwani wa kata ya Mbezi, Ismail Malata alisema kata hiyo imetoka zaidi ya shilingi 4.8 za ujenzi wa mradi wa maji ili kutatua kero ya ukosefu wa maji Kwa baadhi ya mitaa, Billion 3 katika sekta ya Elimu na milioni 500 za ujenzi wa kituo Cha Afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, wilaya ya Ubungo, Meshaki Ole Sabaya alisema CCM wilaya ya Ubungo imepokea maagizo yaliotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi Kwa maslahi mapana ya chama na taifa