Wenye mabasi wapongeza ushirikiano sensa

CHAMA Cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), kimepongeza muitikio wananchi hususani wanachama na watumishi wake kushiriki sensa kuanzia juzi.

Akizungumza Dar es Saalam leo, Mhazini wa chama hicho, Issa Nkya, amesema sensa kama lilivyochukuliwa kwa umuhimu na idadi kubwa ya wananchi, ndivyo ilivyochukuliwa ndani ya TABOA kwa wajumbe wote kukubaliana kuipa kipaumbele.

“Wanachama wote kwa kauli moja tulikubaliana kushiriki kikamilifu zoezi la sensa na tumefanya hivyo, ingawaje idadi ndogo ya baadhi yetu katika maeneo wamesema kuwa bado hawakufikiwa na makarani, tukiamini kuwa watafikiwa kwa kuwa siku bado zipo,” amesema Nkya.

Kwa upande wa watoa huduma wao hususani madereva na wasaidizi wao, Nkya amesema baadhi yao hasa waliokuwa safarini, waliacha taarifa muhimu nyumbani, kabla ya kusafiri na wale waliolala nje ya mikoa  yao walihesabiwa wakiwa huko.

 

Habari Zifananazo

Back to top button