‘Wenye malalamiko fuateni utaratibu kudai fidia’

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imewataka wananchi wapapopata hasara kutokana na kile wanachodai kuwa ni uzembe wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) basi wafuate taratibu kudai fidia.

Meneja wa Ewura Kanda, George Mhina ametoa muongozo huo wakati akizungumza na viongozi maofisa watendaji na madiwani wa kata mbalimbali za Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Mhina amesema zipo taratibu, kanuni na sheria zinazolinda haki ya mteja pamoja na mtoa huduma, hivyo wananchi wanapokuwa na malalamiko ama madai dhidi ya Tanesco wafike Ewura kwa usaidizi.

“Moja ya kazi zetu sisi Ewura ni kushughulikia malalamiko, kwa hiyo kama mtu pengine amepata changamoto wakati wa kupata huduma za mafuta, maji, umeme na gesi afike kwetu kuja kulalamika.

“Utaratibu ni kwamba anaanza kutoa lalamiko lake kwa yule mtoa huduma, na endapo anakuwa hajasikilizwa au amesikilizwa majibu hajaridhika nayo hatua ya pili anakuja kwetu sisi Ewura.

“Kwa hiyo sisi tunalishughulikia kwanza kufanya njia ya usuluhishi, lakini baadaye tunasikiliza kama baraza na haki inapatikana, kuna wengine walishawahi kuunguliwa nyumba tunawapa fidia,” amesema.

Ametolea mfano iwapo mteja amepewa bili kubwa ya maji ama hajaunganishiwa umeme kwa wakati na alishalipia basi basi Ewura wakiarifiwa watatoa maelekezo kwa mamlaka husika, ili kumaliza tatizo.

Ofisa Tawala Msaidizi Wakala wa Huduma kwa Wateja mkoa wa Geita (EWURA CCC), Awadhi Omari amesisitiza Ewura imeandaa mazingira rafiki kushughukia kero zote ili Watanzania wapate huduma stahiki.

Awadhi amewaomba Watanzania wasiwe watu wa kulalamika nyumbani pekee kwa kuwa ipo mamlaka inayowajibika kuwasaidia hivo wawe huru kuelezea kero za watoa huduma.

Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Shinyanga B, wilayani Mbogwe, Abdullah Suleman amekiri Ewura imewafumbua macho kwani Watanzania wengi hawana uelewa sahihi wanapokuwa na malalamiko kwa watoa huduma.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
11 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
11
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x