West Kill Tour kwenye njia za Royal Tour

KATIKA harakati za kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii wa Tanzania Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) imedhamiria kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini kupitia kampeni ya West Kill Tour itakayofanyika Mwishoni mwa mwezi Juni  mkoani Kilimajaro.

TFS  wamesema hayo Juni 14  Dar es salaam,  kuwa wanatekeleza mipango  ya wizara ya maliasili na utalii kama ilivyoainishwa kwenye uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma.

Mratibu wa Kampeni hiyo Mensieur Elly amesema  kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo wanaamini itawavutia watu wengi hivyo kutimiza malengo yao ya kuitangaza Tanzania.

” Tutakuwa na michezo ya kukimbia, kuogelea, mbio za pikipiki, mbio za magari na michezo mingine,ninawakaribisha pia  wawekezaji kwasababu itakuwa ni fursa kwao kutengeneza kipato”  amesema Elly

Kampeni hiyo inatarajiwa kufanyika June 24 na 25 katika msitu wa West kilimanjaro ambapo wageni kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kushiriki katika tukio hilo litakalofanyika kwenye msitu wa West Kilimanjaro uliopo karibu na Mlima Kilimanjaro.

Habari Zifananazo

Back to top button