Wezi fedha za TASAF kushughulikiwa

Wezi fedha za TASAF kushughulikiwa

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya, ameitaka ofisi ya Mkurungezi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaoiba fedha za walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF).

Pia Kyobya amemtaka Mkurungezi huyo kuanisha kaya zenye wazee sana katika manispaa, kusimamia na kuhakikisha fedha za TASAF zinazopelekwa Kwa wazee hao hazipotei.

Ametoa maagizo hayo katika mkutano na walengwa wa TASAF katika kata za Chikongola na Tandika Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoani Mtwara.

Advertisement

Amesisitiza wataalamu wa manispaa kusimamia miradi ya TASAF kwa ufanisi zaidi na kutoa elimu juu ya miradi hiyo, ili faida yake ifahamike na kuwafikia walengwa wote.