Wezi waipa Tanesco hasara milioni 51/-

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Morogoro limepata hasara ya Sh milioni 51.4 kutokana na vitendo vya wizi wa mafuta ya transfoma pamoja na miundombinu mingine katika kipindi cha miezi miwili Agosti na Septemba mwaka huu.

Meneja wa TANESCO mkoa huo, Mhandisi Fadhili Chilombe amesema hayo kwenye taarifa yake katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Morogoro kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.

Mhandisi Chilombe amesema kwa kipindi kisichozidi miezi miwili Agosti 17, 2023 hadi Septemba 29,2023 jumla matukio manne ya kuhujumu transfoma yametokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Manispaa ya Morogoro.

” Ndani ya miezi miwili hujuma za miundombinu ya umeme imefanyika na watu wasiojulikana na hasara iliyopatikana ni Sh 51,476,060. 89″amesema Chilombe .

Meneja wa mkoa amesema, hujuma hiyo ama zinafanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco ama wale waliofanya kazi na kuachishwa,  kwani  wizi huo unafanyika kwa utaalamu mkubwa  kiasi cha kushusha tranfoma, kutengenisha vifaa vyake na kuchukuliwa.

Mhandisi Chilombe amewaomba Wananchi wa mkoa huo kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu  wanaopowaona wanasogelea miundombinu ya umeme katika maeneo yao na kuanza kufanya kazi ili wadhibitishiwe kama ni wametumwa Tanesco au laa.

“Naomba nitoe namba zangu Kwa Umma ,nimeni taarifa kupitia simu yangu 0787 010011 au 0736 010011  mnapoona viashiria vya kufanyika vitendo vya hujuma ,ofisi iweze kujiridhisha hao ni wafanyakazi wa kama wametumwa maeneo hao na watoa taarifa watalindwa.” amesema Mhandisi Chilombe.

Meneja wa Mkoa wa Tanesco amesema hapo nyuma wizi wa miundombinu ya umeme ulikuwa ikifanyika zaidi katika Manispaa ya Morogoro lakini ndani ya wiki hizo umefanyika  pia maeneo ya wilayani ikiwemo wilaya ya Kilosa.

Kwa upande Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kilosa, Mhandisi Daniel Kingu amesema licha ya wizi wa Transfoma pia nguzo nyingi zilichomwa moto  katika Vijiji viwili cha Makwambe ambapo nguzo  26 zimechomwa moto wakati kwenye kijiji  cha Tindiga ni nguzo 16 , na kitendo hicho kimesababisha  vijiji hiyo kukosekana kwa umeme.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work At Home
Work At Home
2 months ago

in just 5 weeks, I worked part-time from my apartment and earned $30,030. After losing my previous business, I quickly became exhausted. Fortunately, I discovered this jobs online, and as a result, I was able to start earning money from home right away. Anyone can accomplish this elite career and increase their internet income by….

After reading this article:…… http://Www.Smartcash1.com

Last edited 2 months ago by Work At Home
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x