Whozu, Billnass, Mbosso wapata ahueni

DAR ES SALAAM; Wasanii Oscar Lelo ‘Whozu’, William Lyimo ‘Billnass’ na Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ wamepata ahueni ya kuondolewa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na muziki iliyokuwa imetolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Novemba 4, mwaka huu.
Hata hivyo wasanii hao hawatajishughulisha na muziki hadi watakapotekeleza adhabu ya kulipa faini walizotozwa na Basata zilizokuwa zikienda pamoja na adhabu za kufungiwa.
Uamuzi huo umefikiwa leo Novemba 14, 2023 kwenye kikao kilichoongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro kilichofanyika ofisi za wizara zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu wa wizara Gerson Msigwa na wasanii hao.
Whozu alitozwa faini ya Sh milioni tatu na Basata, lakini kutokana na uamuzi wa leo atalipa Sh milioni tano, Billnass alitozwa Sh milioni tatu, lakini sasa atalipa Sh milioni moja na Mbosso yeye atalipa Sh milioni tatu. Kulingana na uamuzi wa leo wakitekeleza adhabu hiyo wataendelea na shughuli zao za muziki.
Whozu pia amepewa muda wa saa sita kutekeleza agizo la kushusha wimbo huo kwenye mitandao yake ya kijamii.
Basata ilitangaza kumfungia Whozu miezi sita kutokana na kuchapisha video ya wimbo Ameyatimba aliowashirikisha wasanii hao ambayo inakiuka maadili na ina vitendo vyenye ishara ya matusi. Billnass na Mbosso kila mmoja alifungiwa miezi mitatu.
Akizungumza Dk Ndumbaro amewaasa wasanii na wengine nchini watumie vizuri ubunifu wao kwa kufuata taratibu zilizoanishwa katika mongozo wa uzingatiaji wa maadili katika kazi za Sanaa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EmmaJones
EmmaJones
20 days ago

Making extra salary every month from house more than $15,000 just by doing simple copy and paste like online job. I have received $18,000 from this easy home job. Everybody can now makes extra cash online easily.
.
.
By Just Follow———————————————————>>>  http://Www.BizWork1.Com

Angila
Angila
20 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x