MKOA wa Mtwara unatarajia kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Wiki Viziwi Kitaifa, ambayo yatafanyika Oktoba 26, mwaka huuu.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu: Kujenga Jamii Jumuishi kwa Wote’ yamelenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki ya ustawi kwa viziwi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewaomba wananchi kushiriki maadhimisho hayo, huku akiwahamasiaha pia kuchangia damu na kupima afya zao.
“Natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho hayo, kuchangi damu, kushiriki shughuli za upimaji wa masikio (usikivu), kupata chanjo ya Uviko 19, surua na shinikizo la damu,” amesema na kuongeza kuwa maadminisho hayo yatafanyika Uwanja wa Nagwanda Sijaona.
Maadhimisho hayo ya wiki ya Viziwi hufanyika wiki ya tatu ya mwezi Oktoba kila mwaka na kuandaliwa na Chama Cha Viziwi (CHAVITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.