Wilaya 139 kufikiwa na Mkongo wa Taifa

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania( TTCL) limedhamiria kufanya maboresho makubwa katika sekta ya mawasiliano ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 24, 2023 Jijini Dar es Salaam kwenye Mkutano wa Shirika hilo na Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari ikiwa na tekelezo la agizo la Msajili wa hazina Nehemiah Mchechu la kuzitaka taasisi na Mashirika ya Umma kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga amesema wapo katika mpango mkakati wa kuzimaliza changamoto za kimawasiliano nchini na ilikufikia hilo Wilaya 139 sasa zitafikiwa na huduma ya mkongo wa taifa.

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwezi June 2023, Wilaya 44 zilikwisha fikiwa na Mkongo wa taifa , huku lengo likiwa ni kufikisha Wilaya 100 ifikapo Desemba 2023, na kisha kukamilisha Wilaya 139 mwaka 2024.

Aidha Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wamefanya utafiti wa changamoto za kimawasiliano zinazoyakabili maeneo ya visiwani na wapo tayari kwa utatuzi.

“Tulikuwa na changamoto ya muda mrefu ya kupeleka Mawasiliano Visiwani, mfano Mafia lakini sasa tumepata Suluhisho wataanza kufurahia huduma hizo” amesema Ulanga.

Mkurugenzi wa Biashara TTCL Vedastus Mwita amesema wanaendelea na ujenzi wa Miundombinu huku lengo likuwa ni kufanya vizuri nchi nyingi za Afrika ifikiapo mwaka 2027.

” Kwa miundombinu tunayoiandaa tunatamani kufikia mwaka 2027 muione TTCL ikifanya vizuri nchi mbalimbali Afrika na iweze kushindana na kampuni nyingine zitakazokuwepo” amesema Mwita

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Vyombo vya habari Deodatus Balile amesema mbali na shirika hilo kujikita katika Uwezekaji wa Muindombinu ni lazima wawezeshwe watendaji wa shirika hilo ili kufikia Malengo yao.

Kwa Mujibu wa shirika hilo Mpango mkakati wao unalenga pia kuwa na maendeleo ya uchumi wa kidigitali.

Habari Zifananazo

Back to top button