Wilaya 64 kujengwa VETA

SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2022/23, imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo hivyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Buchosha Erick Shigongo aliyetaka kujua ni lini serikali itajenga chuo cha VETA Wilaya ya Buchosa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kipanga amesema serikali imeshakamilisha kuandaa michoro na upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya ujenzi.

“katika wilaya ya Sengerema eneo lililotengwa kujengwa chuo cha Ufundi Stadi ni katika Kijiji cha Kayenze kata ya Nyehunge na tayari kiasi cha Sh million 45 kimetolewa mwezi Machi, 2023 kwa ajili ya shughuli za awali za ujenzi wa Chuo hicho.” Amesema Kipanga.

Habari Zifananazo

Back to top button