Wilaya ya Tanganyika waja kivingine elimu, afya

Wilaya ya Tanganyika waja kivingine elimu, afya

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, imejiwekea mkakati wa kujenga shule ya mchepuo wa Kingereza (English medium) ili kutatua tatizo la aina hiyo ya shule katika halmashauri hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Shaban Juma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya rasimu ya bajeti katika Kikao cha Kamati ya Ushauri (DCC) Wilaya ya Tanganyika, kilichoongozwa na mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu.

Amesema halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha sh. Bilioni 40.3 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.5 ya bajeti ya mwaka 2022/23 ya Sh.

Advertisement

Bilioni 32.6

Amesema Halmashauri hiyo imepanga kukusanya kiasi hicho cha fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo mapato ya ndani, fedha za ruzuku kutoka serikali kuu na ruzuku kutoka kwa wafadhili na wahisani.

“Kwanza tuna mapato ya ndani ambayo yana jumla ya Sh Bilioni 10 ambayo bajeti hii imeongezeka ukilinganisha na bajeti ya mwaka uliopita, kutokana na kuongezeka kwa bajeti matumizi mengineyo ni asilimia 40 na miradi ya maendeleo itakuwa asilimia 60,” amesema.

Amesema bajeti hiyo imezingatia kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi, ikiwemo kuimarisha sekta ya afya, elimu na maliasili.

Katika sekta ya afya halmashauri imepanga kuboresha Kituo cha Afya Sibwesa kuwa cha mfano, kuboresha Hospitali ya Ikola na sekta ya maliasili kuanzisha kituo cha nyuki cha kuchakata asali sambamba na kukarabati nyumba zipatazo 14 za halmashauri zilizopo Mpanda mjini.

Kwa upande wake Buswelu amehimiza kupanga mipango madhubuti ya ukusanyaji mapato ili kufikia azma ya utekelezaji wa miradi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *