Wivu wa mapenzi waua mke, mume

MOROGORO; Devotha Gilbert (20) ,mfanyabiashara na mkazi wa Kata Mwembesongo mkoani Morogoro, anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali mwili mwake na mumewe, kisha mwili wake kutelekezwa eneo la Mafisa Kwa Kambi, Manispaa ya Morogoro.

Baada ya kudaiwa kufanya mauaji ya mkewe kijana huyo Boniface John (26), ambaye ni mfanyabiashara wa machinjio ya mbuzi, Kata ya Kichangani, Morogoro, aliondoka na pikipiki yake na kuelekea mtaa wa Kindibwa, Kata ya Bigwa, Morogoro na kujiua kwa kujichoma kisu shingoni na tumboni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 12, 2023 na chanzo cha vifo hivyo ni wivu wa mapenzi.

“Chanzo cha vifo hivi vya wanandoa ni wivu wa mapenzi na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, “ amesema Kamanda Mkama.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button