Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imeingia makubaliano na Taasisi ya Tanzania Startups Association (TSA) kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya kisera na kisheria kwa ajili ya Startups.
Mazingira hayo yatasaidia Startups kukua, kuvutia wawekezaji, kuvutia mitaji lakini pia bidhaa na huduma zao kupata masoko ndani na nje ya nchi. Wizara imewakilishwa na Katibu Mkuu Dk Jim Yonaz na TSA imewakilishwa na Mtendaji Mkuu Zahori Muhaj.