Wizara ya afya inafuata miongozo ya WHO-Ummy

WIZARA ya Afya imesema inafuata miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo inasema afya ni ukamilifu wa binadamu kimwili, kiakili, kijamii na kutokuwepo kwa magonjwa ambapo sera hiyo inataka huduma itolewe kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtu.

Waziri mwenye dhamana, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Februari 12, 2024 bungeni jijini wakati akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati kwa mwaka 2023 katika Bunge la 12, mkutano wa 14 kikao cha 10 jijini Dodoma na kujibu hoja ya Luaga Mpina ya kutaka kujua kama ni kipaumbele cha kutoa huduma za kuongeza makalio.

“Mhe. Mwenyekiti watu wanakwenda kutafuta huduma ya kuongeza makalio nchi za nje na wanaenda kulipa dola, kwanini hizi dola zisibakie ndani ya nchi na watoa huduma wetu wanaweza kutoa huduma hizo.” Amesema Waziri Ummy.

Advertisement

Amesema fedha hizo ndizo zinazotumika kutoa huduma za msamaha kwa wasiojiweza, lakini pia ndio tunatumia kutibia mama wajawazito pamoja na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.