Wizara ya Afya yamuonya Haji Manara

DAR ES SALAAM: WIZARA ya Afya, imemtaka Haji Manara kuacha kutumia ushawishi wake mtandaoni kwa kutumia taarifa za afya kwa madhumuni ya dhihaka, ikiwemo utani wa jadi.

Mapema leo Haji alichapisha video katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha Waziri @wizara_afyatz @ummymwalimu akieleza kuzuka kwa ugonjwa wa Mgunda, ambapo ukurasa wa @wizara_afyatz umejibu chapisho hilo ikieleza kuwa video hiyo sio ya sasa.

“Salamu @hajimanara Tumeona habari hiyo ambayo inazunguka mitandaoni kuonesha utani wa jadi wa mpira kati ya Timu za @simbasctanzania na @yangasc ukihusisha jina la Kocha Mgunda,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kupakia video hiyo mtandaoni inaweza pokelewa tofauti na watu wengine na kuzua taharuki juu ya mlipuko wa Ugonjwa wa Mgunda.

“Kutokana na ushawishi ulionao ndani ya jamii wapo watu wengine wanaweza jua kuwa ugonjwa huo umeibuka tena na sio ujumbe uliokusudia wa utani wa mpira,

“Ni vyema ukaelezea kuwa video hiyo ni ya muda na hakuna ugonjwa wa Mgunda nchini au kuitoa na kutumia maudhui mengine.”

Hata hivyo mpaka HabariLEO inapakia chapisho hili bado hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Manara.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7BvzU6od9Y/?img_index=1

Soma pia: https://habarileo.co.tz/diamond-akerwa-wanaomponda-haji-manara/

Habari Zifananazo

Back to top button