Wizara ya Fedha yaliomba Bunge Sh tril.18.17

DODOMA; WIZARA ya Fedha imeomba Bunge liidhinishe matumizi ya jumla ya Sh trilioni 18.7 kwa mwaka wa fedha 2024.25.

Akiwasilisha bungeni leo Juni 4, 2024, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema:

“Kwa mwaka 2024/25, Wizara ya Fedha inaomba kuidhinishiwa matumizi ya jumla ya shilingi trilioni 18.17 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu nane (8) ya kibajeti,” amesema Waziri Nchemba.

Katika hotuba yake ametaja vipaumbele vya mafungu ya Wizara ya Fedha, ambavyo ni: Kutafuta na kukusanya mapato ya Sh trilioni 44.19 kati ya maoteo ya Sh trilioni 49. 35 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Serikali.

“Kuimarisha na kusimamia mifumo ya mapato, matumizi na mali za Serikali ikiwemo IDRAS, TANCIS, MUSE, NeST, CBMS na GAMIS.

“Kuhudumia deni la Serikali kwa wakati na kuboresha kanzidata ya kutunza taarifa za deni.

“ Kutoa elimu ya huduma za fedha kwa wananchi kwa lengo la kukuza huduma jumuishi za fedha nchini.

“Kujenga uwezo kwa wakaguzi wa ndani, kamati za ukaguzi pamoja na waratibu wa usimamizi wa vihatarishi katika taasisi za umma,” amesema Waziri Nchemba.

Habari Zifananazo

Back to top button