Wizara ya Habari yaomba kuidhinisha Sh bilioni 212

WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imeomba kuidhinisha Sh bilioni 212.457.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametoa mchanganuo wa fedha hizo kama ifuatavyo.

Nape amesema Sh bilioni 30.503 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Sh bilioni 18.522 ni za mishahara na Sh bilioni 11.981 ni za matumizi mengineyo.

Aidha, Sh bilioni 181.953 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo Sh bilioni 146.777 ni fedha za ndani na Sh bilioni 35.176 ni fedha za nje.

Habari Zifananazo

Back to top button