Wizara ya kilimo yafungua fursa kilimo cha Chai

DAR ES SALAAM: NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Hussein Mohamed Omar amewataka viongozi pamoja na wakulima kuendelea kuongeza ujuzi wa kuzalisha chai iliyo bora na Kuweka mikakati ya ushiriki wa minada ya kuuza chai.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa kwanza wa kimataifa wa chai Naibu katibu mkuu, amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya mwongozo wa Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira wezeshi kwa wakulima na wawekezaji kuwekeza katika zao la chai.

Omar amesema mnada huo unaolenga kuongeza thamani kwenye zao la chai nchini ili lichangie kikamilifu kwenye pato la taifa.

“Ili kuhakikisha adhma hiyo inatimia ni lazima TBT kuhakikisha kuwa inatekeleza wajibu wake wa ufanisi kwa kuchochea mashirikiano mazuri na nchi jirani inayozalisha zao la chai na kuhamasisha kutumia mnada wa hapa nchini, hivyo endeleeni kushirikisha sekta binafsi katika maendeleo ya zao la chai, lakini pia kuhakikisha viwanda vya chai vinawalipa kwa wakati wakulima ili kuwahamasisha kulima.” amesema Omar

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TBT, Mary Kipeja amesema kuwa katika kuhakikisha mnada huo unazidi kuwa na tija kwa taifa tayari zipo hatua za awali ambazo zimeshaanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kusimamia ukarabati wa mitambo kwenye viwanda vya chai nchini pamoja na kuanzishwa kwa kampuni ya Chai ya Kilolo, Kilolo Tea Company (KTC).

Kipeja amesema mnada huo utaenda kuongeza kipato cha wakulima wa chai, kuongeza ajira kwa wakulima za moja kwa moja na taifa kwa ujumla.

 

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button