Wizara ya kilimo yatakiwa kuongeza wakala wa mbolea

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo ameitaka Wizara ya Kilimo kuongeza vituo vya mawakala wa kuuza mbolea nchini kwani wananchi wanatoa fedha nyingi kugharamia mbolea kuwafikia.

Agizo hilo amelitoa leo akiwa Kijiji cha Mtinko wilayani Singida baadaNa ya wananchi wa eneo hilo kulalamika mbolea ya ruzuku wanaipata kwa kupanga foleni na wakati mwingine baadhi yao hawana taarifa ya ujio wake.

“Pembejeo za kilimo ni changamoto hususan mbolea,ugawaji wake kwa hapa ni kupanga foleni na kuuziwa kwa bei kubwa kutokana na umbali inafika hadi shilingi 100,000 kwa mfuko,amesema Amon Lunde”.

Amesema wanaomba vituo vya mawakala kuuzia mbolea hiyo viongezwe kwani hivi sasa ni vichache na mahitaji ya mbolea ni makubwa kwa wakulima ambao wamehamasika kulima kwa tija.

Akijibu hoja hiyo Chongolo ameagiza wizara ya kilimo kuhakikisha wanaongeza mawakala wa mbolea nchini ili wawafikie wakulima wengi na waondokane na adha ya umbali unaochangia gharama za mbolea kuongezeka.

Habari Zifananazo

Back to top button